Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kujiondoa kwa Canada kutoka kwa makubaliano ya Kyoto ni hatua ya kujutia:UM

Kujiondoa kwa Canada kutoka kwa makubaliano ya Kyoto ni hatua ya kujutia:UM

Mkuu wa masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa kwenye Umoja wa Mataifa Christiana Figueres amesema kuwa hatua ya kujiondoa kwa Canada kutoka kwenye makubaliano ya Kyoto ni jambo la kujutia na kuyataka mataifa yaliyostawi kutekeleza ahadi yaliyotoa kwenye mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa ulioandaliwa mjini Durban nchini Afrika Kusini.

Amesema kuwa mataifa yaliyoendelea yanahitaji kuwa kwenye mstari wa mbele katika kupunguza hewa chafu na kuzisaidia nchi zinazoendelea kuwekeza kwenye kawi isiyochafua mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa ambazo tayari zimeanza kuonekana.