Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Njaa yazidi kuchacha nchini Niger huku bei ya vyakula ikipanda

Njaa yazidi kuchacha nchini Niger huku bei ya vyakula ikipanda

njaa nchini NigerShirika na mpango wa chakula duniani WFP linasema kuwa ukame ambao umelikumba eneo la Saleh Magharibi mwa Afrika umewaacha wenjeji wakisumbuliwa na njaa kwa mara ya tatu sasa kwa muda wa miaka kumi.

 Hali hii umewafanya wenyeji kushindwa kujikuamua kutoka kwa janga la awali la njaa suala lililwafanya kuuza mifugo wao. Nchini Niger mvua kidogo na wadudu waharibifu vimechangia kupungua kwa mavuno na kusababisha kupanda kwa bei ya vyakula.

Kwa sasa WFP inapanga kuongeza oparesheni zake ili kuwafikia watu milioni 3 walioathiriwa na njaa. Gaëlle Sévenier kutoka WFP anasema kuwa hatua za haraka zinahitaji kuchukuliwa ili kuzuia kusambaa kwa janga hilo.

CLIP