Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bendera ya Palestina yapandishwa kwenye makao makuu ya UNESCO

Bendera ya Palestina yapandishwa kwenye makao makuu ya UNESCO

Bendera ya utawala wa Palestina imepandishwa kwenye mlingoti katika makao makuu ya shirika la Elimu, Sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO kama ishara ya kukubaliwa kwake kwenye shirika hilo. Palestina ilichaguliwa mwanachama wa 195 wa UNESCO mwezi Oktoba mwaka huu.

Rais wa mamlaka ya wapalestina Mahmoud Abbas alihudhuria sherehe hizo akiwemo pia mkurugenzi mkuu wa UNESCO Irina Bokova. Mr. Elias Sanbar, mwakilishi wa kudumu wa Palestina kwenye shirika la UNESCO na amezungumza na Madiha Sultan wa Redio ya UM ambapo ameelezea furaha yake kufuatia kujinga huko

UNESCO ndilo shirika la kwanza la Umoja wa Mataifa kuikubali Palestina kuwa mwanachama wake.