ICC yaliarifu Baraza la Usalama namna Malawi ilishindwa kumkamata rais wa Sudan

13 Disemba 2011

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu dhidi ya binadamu ICC imetoa taarifa ikiielezea namna serikali ya Malawi ilivyoshindwa kutoa ushirikiano kutokana na hatua yake ya kupuzia mwito wa kumkamata Rais wa Sudan Omary al-Bashir ambaye hivi karibuni alizuru nchi hiyo.

Malawi ambaye ni mwitifaki wa mkataba wa Rome unaotambua kuundwa kwa mahakama hiyo ilipuzilia mbali miito toka jumuiya kimataifa iliyotaka imkamate kiongozi huyo wa Sudan ambaye anatakiwa na mahakama ya kimataifa juu ya uhalifu uliofanyika huko Darfur.

Kutokana na uamuzi huo uliochukuliwa na serikali ya Malawi,ICC imesema kuwa imeliarifu baraza la usalama pamoja na taasisi nyingine ambazo zinatambua mahakama hiyo.

Majaji wa mahakama hiyo wamesema Malawi haikuwa na kikwazo chochote kutotekeleza sheria za kimataifa kwa kumkamata kiongozi huyo bali iliamua kuchukua mkondo unaofuatwa na serikali nyingine za kiafrika.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter