Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa UM ataka kudhibiti uwezo wa makampuni yanayonunua madeni kuzishitaki nchi masikini

Mtaalamu wa UM ataka kudhibiti uwezo wa makampuni yanayonunua madeni kuzishitaki nchi masikini

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu madeni ya nje na haki za binadamu Cephas Lumina, leo ameitaka serikali ya Jersey kupitisha sheria sawa na ile iliyoidhinishwa na Uingereza mwaka jana ya kudhibiti uwezo wa makampuni ya biashara yanayonunua madeni kuweza kuzishitaki nchi masikini zilizo na mzigo mkubwa wa madeni katika mahakama zake.

Amesema tabia hiyo ya makampuni vyombo vya fedha kununua madeni ijulikanayo kama “Vulture funds” inazinyima haki nchi masikini kufaidika na juhudi za kufutiwa madeni ambazo zina lengo la kuboresha huduma za jamii kama kupata maji safi ya kunywa, huduma za afya, elimu na nyumba bora. Bwana Lumina ameongeza kuwa jumuiya ya kimataifa isikubali hali hii ambayo inazikandamiza nchi masikini zenye madeni. Alice Kariuki na taarifa kamili.

(ALICE KARIUKI NA TAARIFA KAMILI)