Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa Malaria vimepungua

Vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa Malaria vimepungua

Kulingana na ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa ni kuwa vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa Malaria vimepungua kwa zaidi ya asilimia 25 tangu mwaka 2000. Kulingana na ripoti iliyotolewa na shirika la afya duniani WHO ni kuwa kuliripotiwa kesi milioni 216 za ugonjwa wa malaria huku watu 600,000 wakifa kutokana na ugonjwa huo mwaka 2010.

Ripoti hiyo pia inasema kuwa kati ya nchi 99 zenye visa vya Malaria 43 kati yao ziliandikisha kupungua kwa visa hivyo kwa zaidi ya asilimia 50 kwa muda wa miaka kumi iliyopita. Robert Newman ni mkurugenzi wa programu za malaria kwenye WHO.

(SAUTI YA ROBERT NEWMAN)