Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Manyota wa soka kuchangisha fedha kusaidia pembe ya Afrika

Manyota wa soka kuchangisha fedha kusaidia pembe ya Afrika

Baadhi ya manyota wa kandada duniani wakiwemo Robaldo, Zinedine Zidane na Didier Drogba watashiriki kwenye mechi ya kirafiki hii leo yenye lengo la kuchangisha fedha za kusaidia eneo la pembe ya Afrika.

Mechi hiyo ya kupiga vita umaskini ni kati ya klabu ya ujerumani Hamburger Sport-Verein dhidi ya blabu iliyobuniwa na Zidane, Ronaldo na Drogba. Manyota hao watatu ni mabalozi wema kwa shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP. Aziyadé Poltier-Mutal kutoka UNDP anasema kuwa tikiti 30,000 zinatarajiwa kuuzwa wakati wa mechi hiyo.

(SAUTI YA AZIYADE POLTIER-MUTAL)