Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwafrika wa kwanza achaguliwa kuwa mwendesha mashitaka mkuu wa ICC

Mwafrika wa kwanza achaguliwa kuwa mwendesha mashitaka mkuu wa ICC

Mwanamke wa Kigambia amekuwa Mwafrika wa kwanza kuteuliwa kushika wadhifa wa mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC yenye makao yake makuu The Hague Uholanzi.

Fato Bensouda amekuwa akifanya kazi kama naibu mwendesha mashitaka tangu mwaka 2004 na kabla ya hapo alikuwa akifanya kazi kama mshauri na wakili wa kesi kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa mauaji ya Rwanda iliyoko Arusha Tanzania.

Uteuzi wake umeidhinishwa Jumatatu na Baraza Kuu mjini New York. Mwendesha mashitaka mkuu wa sasa Luis Moreno Ocampo kutoka Argentina atachia madaraka Juni mwakani baada ya kushika wadhifa huo kwa miaka 9.