Nchi zinazoendelea zinakabiliwa na wimbi jipya la uharamia wa kimtandao :UM

12 Disemba 2011

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa nchi zinazoendelea huenda sasa zikakabiliwa na hali ngumu ya uhalifu wa kimtandao na kusisitiza haja ya kuibuliwa kwa mbinu za haraka za kukabiliana na wimbi hilo jipya.

Akizungumzia hali hiyo Rais wa Baraza la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya uchumi na jamii ECOSOC Bwana Lazarous Kapambwe amesema kuwa iko haja ya kusaka mbinu za haraka kukabili wimbi hilo jupya kwa nchi zinazoendelea.

Amesema kuwa uharamia wa kimtandao ni janga linaloliandama nchi zinazoendelea kwa wakati huu na kuonya kwamba kama kutakoseka kwa utashi wa pamoja kukabiliana na wimbi hilo basi kunaweza kushuhudiwa ustawi mbaya miongoni mwa nchi husika. Ametaka mafungamano ya pamoja ikiwemo kupigwa kwa jeki kwenye maeneo ya kitaalumu ili kudhibiti kasi yake.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter