Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban awataka vijana kushiriki katika kuilinda dunia

Ban awataka vijana kushiriki katika kuilinda dunia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa vijana kusaidia kupunguza changamoto zinazoikumba dunia zikiwemo za mabadiliko ya hali ya hewa ili kuvihakikisha maisha mema vizazi vinavyokuja.

Akizungumza alipokuwa akihutubia kundi la vijana kwenye kongamano moja mjini Dohar Qartar Ban amewaambia kuwa hakuna ulimengu mwingine isipokuwa huu tu na ni lazima ulindwe. Ban pia aliwakaribisha vijana kujiunga na Umoja wa Mataifa katika kampeni zake kwa minajili ya kuunga mkono amani , haki za binadamu pamoja na kwenye utunzi wa mazingira.