Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Baraza Kuu alaani shambulio dhidi ya walinda amani wa UM Lebanon

Rais wa Baraza Kuu alaani shambulio dhidi ya walinda amani wa UM Lebanon

Rais wa Baraza Kuu wa Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser Jumatatu ameongeza sauti yake katika kulaani shambulio dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa lililofanyika mwishoni mwa wiki.

Walinda amani watano wa mpango wa Umoja wa Mataifa Lebanon UNFIL na raia wawili walijeruhiwa bomu liliporipka wakati gari la Umoja wa Mataifa likipita kwenye mji wa Tyre.

Katika taarifa yake Bwana Al-Nasser amekaribisha ahadi ya serikali ya Lebanon ya kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria waliohusika na uasi huo. Amezitaka pande zote kuzingatia usalama wa walinda amani wa UNIFIL na wafanyakazi wa mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa kwa mjibu wa sheria za kimataifa.

UNFIL ambayo imekuwepo Lebanon tangu mwaka 1978 ina walinda amani zaidi ya 12,000 kutoka mataifa 35.