Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufisadi unaathiri upatikanaji wa ardhi na maendeleo:FAO

Ufisadi unaathiri upatikanaji wa ardhi na maendeleo:FAO

Kuna shinikizo kubwa lisilostahili katika masuala ya ardhi wakati maeneo mengi yakilimwa, kuchukuliwa kwa ajili ya upanuzi wa miji au kutelekezwa kutokana na mmomonyoko wa udongo, mabadiliko ya hali ya hewa na vita.

Hayo yamo kwenye ripoti ya pamoja ya shirika la chakula na kilimo FAO na shirika la kimataifa la kupambana na ufisadi Transparency International.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo maendeleo haya yameongeza shinikizo katika sheria, mchakato na taasisi zinazoamua ardhi ipi itumike, na nani?, kwa muda gani na kwa masharti gani. George Njogopa na maelezo kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)