Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yaongoza kujifunza kwa mafunzi kupitia simu za mkononi

UNESCO yaongoza kujifunza kwa mafunzi kupitia simu za mkononi

Wiki ya kwanza ya kujifunza kwa njia ya simu iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO kwa ushirikiano na kampuni ya simu za mkononi ya Nokia imeanza Jumatatu mjini Paris Ufaransa makao makuu ya shirika hilo.

Katika juma zima lililowaleta pamoja wataalamu wa elimu mjadala utahusu matumizi ya teknolojia ya simu katika elimu kwa kutumia wataalamu wa kimataifa. Katika mkutano huo utakaofuatiwa na kongamano hadi Desemba 16 wadau mbalimbali wataangalia umuhimu na changamoto za kujifunza kupitia simu za mkononi katika wakati huu ambapo watu zaidi ya bilioni 5.3 duniani wana simu za mkononi ikiwa ni sawa na asilimia 90 ya watu wote duniani.

UNESCO inasema teknolojia ya simu za mkononi sio tuu inaongeza fursa ya watu kupata taarifa na elimu, lakini pia inaweza kubadili elimu yenyewe kwa kutoa mifumo mipya ya kufuta ujinga na mifumo mipya ya kufundisha na kujifunza.