Uchaguzi wa bunge Ivory Coast umefanyika kwa utulivu lakini wapinzani waugomea

12 Disemba 2011

Duru za habari kutoka nchini Ivory Coast zinasema uchaguzi wa ubunge wa Jumapili umefanyika kwa utulivu huku kitengo cha upinzani kikiugomea uchaguzi huo hakikuathiri nia ya watu kupiga kura kwa mara ya kwanza baada ya muongo.

Kwa mujibu wa mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Bert Koenders kwa ujumla uchaguzi umefanyika kwa amani kutokana na hali aliyoishuhudia alipozuru vituo mbalimbali vya upigaji kura mjini Abidjan na maeneo mengine. Maafisa wa uchaguzi wanasema wanatarajia matokeo mengi ya uchaguzi huo siku ya Jumanne. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter