Mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa wamalizika kwa matumaini:UNEP

Mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa wamalizika kwa matumaini:UNEP

Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP limesema mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa mjini Durban umemalizika Jumapili kwa matumaini ya hatua za kusonga mbele kuinusuru dunia.

Hatua kadhaa muhimu zimeafikiwa ikiwemo muafaka wa majadiliano mapya na mkataba utakaojmuisha kila upande na pia kuanzishwa kwa mfuko wa hali ya hewa unaojali mazingira yaani Green Climate Fund.

Hata hivyo UNEP inasema matokeo ya mkutano huo wa Afrika ya Kusini yameiacha dunia na changamoto kubwa kama kweli wanataka kukiweka kiwango cha joto duniani kuwa chini ya nyuzi joto mbili katika karne hii ya 21.