Mkutano wa Durban umetoa muelekeo wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa:UNFCCC

Mkutano wa Durban umetoa muelekeo wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa:UNFCCC

Mataifa yaliyokutana mjini Durban Afrika ya Kusini kwa ajili ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa yametoa muongozo wa hatima ya jumuiya ya kimataifa katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, huku yakitambua haja ya haraka ya kuongeza juhudi za pamoja za kupunguza gesi ya viwandani na kuhakikisha kiwango cha joto cha dunia kinasalia chini ya nyuzi joto mbili.

Hayo yamesemwa na kitengo cha Umoja wa Mataifa cha mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa UNFCCC. Kwa mujibu wa waziri wa Afrika ya Kusini wa uhusiano wa kimataifa na ushirikiano Maite Nkoana-Mashabane ambaye pia alikuwa raia wa mkutano huo wa COP 17, hatua kubwa zimepigwa kwenye mkutano za kusonga mbele kwa pamoja. Amesema anaamini kwamba kile kilichoafikiwa Durban kitakuwa na jukumu kubwa katika kuiokoa dunia ya kesho leo katika mabadiliko ya hali ya hewa.

(SAUTI YA MAITE NKOANA-MASHABANE)