Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muungano wa ustaarabu unachangia katika mustakhabali wa dunia:Ban

Muungano wa ustaarabu unachangia katika mustakhabali wa dunia:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema amebaini fursa tano muhimu za maamuzi ya kuunda mustakhabali wa dunia katika miongo ijayo. Amesisitiza kwamba muungano wa ustaarabu una nafasi kubwa katika ajenda hiyo.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa kongamano la Umoja wa Mataifa la muungano wa ustaarabu mjini Doha Qatar Ban amesema fursa ya kwanza ni kuwawezesha wanawake na vijana, pili kuzuia migogoro na ghasia, tatu kujenga dunia salama na huru, nne ni kuyasaidia mataifa katika kipindi cha mpito hususan nchi za Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini na mwisho ni kuhakikisha maendeleo endelevu yanaduumishwa. Hayo ndio mambo ya kuyapa kipaumbele katika miaka ijayo amesisitiza Ban.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)