Mlipuko wa bomu Lebanon Kusini wajeruhiwa walinda amani watano wa UM

9 Disemba 2011

Walinda amani watano wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon wamejurhiwa baada ya bomu lililokuwa likilenga gari lao kulipuka Kusini mwa nchi hiyo mapema leo.

Gari hilo la mpango wa Umoja wa Mataila Lebanon UNFIL lilikuwa likisafiri kusini nje kidogo ya mji wa bandari wa Tyre wakati likipolengwa kwa mujibu wa mpango huo.

Walinda amani waliojeruhiwa walipatiwa matibabu katika eneo la tukio na kisha kusafirishwa kwenda kupata matibabu zaidi.

UNFIL inasema timu yake ya uchunguzi hivi sasa inashirikiana na jeshi la Lebanon kupata ukweli na mazingira ya shambulio hilo. UNFIL imekuwepo Lebanon tangu mwaka 1978 na ina walinda amani zaidi ta 12,000 kutoka nchi 35.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter