Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tshisekedi apinga matokeo ya uchaguzi yanayosema Kabila ni mshindi DRC

Tshisekedi apinga matokeo ya uchaguzi yanayosema Kabila ni mshindi DRC

Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameanza kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge uliofanyika mwezi uliopita. 

Matokeo hayo yalitarajiwa kutoka siku ya Jumanne wiki hii lakini maafisa wa uchagzi wanasema matatizo ya kusambaza vifaa katika nchi hiyo kubwa ndio yalisababisha ucheleweshaji wa kutolewa matokeo hayo. 

Huku asilimia 90 ya kura zote zikiwa zimehesabiwa, tume ya uchaguzi inasema Rais wa sasa Joseph Kabila ndiye anayeongoza kwa asilimia 49 dhidi ya asilimia 33 ya mpinzani wake mkuu, Etienne Tshisekedi. Mshauri wa Rais Kabila Aubin Minaku alikuwa na haya ya kusema baada ya kutangazwa matokeo hayo. 

(SAUTI YA AUBIN MINAKU) 

Hata hivyo mpinzani huyo Tshisekedi ameyapinga matokeo hayo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi. 

(SAUTI YA TSHISEKEDI) 

Tume ya uchaguzi imesema hali ya usalama imeimarishwa iwapo patatokea ghasia zozote kufuatia madai ya udanganyifu katika uchaguzi huo.