Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNHCR apongeza hatua kwenye suala la wasiokuwa na utaifa

Mkuu wa UNHCR apongeza hatua kwenye suala la wasiokuwa na utaifa

Kamishina mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameyapongeza mataifa yaliyohudhuria mkutano wa Geneva kuhusu ukosefu wa utaifa kwa kupiga hatua kubwa mbele.

Akiongea kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na waakilishi kutoka karibu mataifa 150 Guterres amesema kuwa hatua zilizopigwa ni muhimu kwa kuwalinda wasio na utaifa. Guterres ameongeza kuwa tayari nchi nane zimeidhinisha mikataba kuhusu wasio na utaifa mwaka huu huku nchi 20 zikitoa ahadi kwenye mkutano wa mawaziri kuhusiana na kuidhinishwa kwa mikataba hiyo.