Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misitu kwenye milima iko hatarini:FAO

Misitu kwenye milima iko hatarini:FAO

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO linasema kuwa kuendelea kuwepo kwa misitu ya milima ni jambo linalotajwa kuwa kwenye hatari kutokana na kupanda kwa joto na moto wa msituni, kuongeza kwa idadi ya watu na kuendelea kuwepo ukosefu wa chakula na mafuta. FAO inasema kuwa kuongezeka kwa watu pamoja na sekta ya kilimo vimewalzimu wakulima wadogo kuhamia milimani suala ambalo limechangia kuwepo uharibifu wa misitu.

Kulingana na ripoti ya FAO ni kwamba huenda mabadiliko ya hali ya hewa yakachangia kuoungezeka kwa wadudu waharibifu na magonjwa masuala ambayo yatachangia kutoweka kwa misitu sehemu zenye milima. Flora Nducha na taarifa kamili.

(RIPOTI YA FLORA NDUCHA)