Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu ya UM na hukumu kali nchini Thailand

Ofisi ya haki za binadamu ya UM na hukumu kali nchini Thailand

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea kushangazwa kwake na kesi pamoja na hukumu kali dhidi ya watu walioenda kinyume na utawala nchini Thailand na athari za kesi hizo dhidi ya haki ya kusema. Wakati ofisi hiyo ikielezea wasi wasi wake pia inautaka utawala nchini Thailand kufanyia marekebisho sheria hizo.