Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa Durban watakiwa kungazia athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa uhamiaji

Mkutano wa Durban watakiwa kungazia athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa uhamiaji

Mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM William Lacy Swing ameutaka mkutano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa unaoendelea mjini Durban nchini Afrika Kusini kulipa kipaumbele suala la athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa uhamiaji.

Mwaka mmoja baada ya makubaliano ya mkutano wa Cancun ambapo serikali zilitakiwa kuchukua hatua kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa bado ni machache yaliyotekelezwa. Bwana Swing ameelezea umuhimu wa mataifa wa kuwalinda watu walioathirika na mabadiliko ya hali ya hewa. Jumbe Omari Jumbe ni afisa mawasiliano wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)