Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka 2011 umekuwa tofauti kwa haki za binadamu:Pillay

Mwaka 2011 umekuwa tofauti kwa haki za binadamu:Pillay

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuwa mwaka wa 2011 umekuwa mwaka usiokuwa wa kawaida kwenye masuala ya haki za binadamu. Akiongea kabla ya maadhamisho ya siku ya kimataifa ya haki za binadamu Pillay amesema kuwa mwaka 2011 ni mwaka ambao neno moja kutoka kwa kijana mmoja kijijini nchini Tunisia lilichangia kwenye mabadiliko makubwa.  

Baada ya majuma manne tu lilisabababisha kutimuliwa madaraka kwa utawala dhalimu. Pillay ameongezeka kuwa yalitokea mjini Tunis yalisambaa kwenda Cairo na miji mingine mingi katika eneo hilo ambapo amelitaja neneo hilo kuwa lenye hadhi.