Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Burundi inapiga hatua kuimarisha amani-UM

Burundi inapiga hatua kuimarisha amani-UM

Burundi imetajwa kupiga hatua kubwa juu ya uimarishwaji wa amani na mshikamano baada ya kuvuka kipindi kigumu cha machafuko na vita, kipindi ambacho kilishuhudia utengamao wa mambo mbalimbali ukiporomoka.

Kulingana na mwanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa, pamoja na changamoto kadhaa zilizosalia lakini hata hivyo taifa hilo limefanikiwa kusimama kidete kulinda amani yake.

Karin Landgren amesema kuwa hata hivyo taifa hilo linapaswa kuongeza juhudu ili kuiondoa mikwamo inayojitokeza kwenye maeneo ya kiuchumi na ustawi wa kijamii ili kuharakisha mageuzi ya kulibadli maisha ya wananchi wa Burundi. Lakini ameonya kuwa maouji yanayojitokeza katika siku za hivi karibuni yakiwa na mkono wa kisiasa yanaweza kurudisha nyuma hatua muhimu zilizopigwa na taifa hilo.