Kampeni ya siku ya haki za binadamu kupitia mitandao yashika kasi

8 Disemba 2011

Kampeni ya kuchagiza mkataba wa kimataifa wa haki za binadamu kupitia mitandao ya kijamii imeshika kasi huku zikiwa zimesalia siku mbili tuu kabla ya siku ya kimataifa ya haki za binadamu inayoadhimishwa kila mwaka Desemba 10.

Hayo yamesemwa Alhamisi na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ambaye inasema imeongeza wafuasi wanaojadili masuala ya haki za binadamu kupitia mitandao kama facebook na twitter kwa lugha mbalimbalizikiwemo Kiingereza, Kifaransa, Kihisoania na Kichina. Kampeni hiyo inaitwa ‘siku 30 na haki 30”. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter