Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwendesha mashitaka wa mahakama ya Yugoslavia ya zamani ataka

Mwendesha mashitaka wa mahakama ya Yugoslavia ya zamani ataka

Mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu kwa ajili ya Yugoslavia ya zamani ICTY amewasilisha ripoti yake ya mwaka kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatano jioni.

Serge Brammertz ameuambia ujumbe wa Baraza la Usalama kwamba hatua kubwa iliyopigwa tangu mwaka jana na mahakama hiyo ni kukamatwa kwa muhalifu aliyekwa mafichoni Goran Hadzic hapo Julai 20. Kwa kukamatwa kwa Hadzic sasa hakuna hata mmoja kati ya watu 161 walioshitakiwa na mahakama hiyo ambaye hajapatikana. Lakini ameonya bado kuna changamoto zingine.

(SAUTI YA SERGE BRAMMERTZ)

Brammertz amezitolea nchi wito wa kuonyesha moyo wa kuhakikisha haki inatendeka kimataifa kama ilivyodhihirishwa na mahakama ya ICTY.