Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tatizo la utapiamlo uliokithiri limepungua kidogo:OCHA

Tatizo la utapiamlo uliokithiri limepungua kidogo:OCHA

Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Umoja wa Mataifa kuhusu lishe umeonyesha kwamba kimataifa kuna kuimarika kidogo katika kiwango cha utapiamlo uliokithiri, pamoja na kupungua kwa idadi ya vifo vya watoto Kusini mwa Somalia.

OCHA ambalo ni shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura limesema licha ya mafanikio hayo kidogo bado fedha zaidi zinahitajika Somalia kushughulikia matatizo mengine ya kibinadamu na lina mpango wa kutoa ombi la kimataifa la dola bilioni 1.5 kuisaidia Somalia mwaka 2012 ombi litakalozinduliwa rasmi Desemba 13 mjini Nairobi Kenya.

Rita Maingi afisa mawasiliano wa OCHA anasema suala la utapia mlo limekuwa likiisumbua Somalia kwa muda na kupungua japo kiasi ni hatua muhimu.

(SAUTI YA RITA MAINGI)

Ameongeza kuwa mva kubwa zinazonyesha bonde la mto Juba na Kusini mwa Somalia zimesababisha mafuriko maeneo ya Gedo na Lower Juba na kuwa vigumu kufikisha msaada kwa watu wanaouhitaji. Pia OCHA inatathimini athari kwa watu milioni 3 wanaohitaji msaada baada ya NGO’s na mashirika 16 ya Umoja wa Mataifa ya misaada kupigwa marufuku na Al Shabaab.