Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misaada pekee haitoshi kushughulikia mahitaji ya nchi maskini:EU

Misaada pekee haitoshi kushughulikia mahitaji ya nchi maskini:EU

Nchi zinazoendelea zina umiliki na jukumu la kwanza kwa ajili ya mafanikio na maendeleo yao. Balozi Thomas Mayr-Harting mkuu wa ujumbe wa Muungano wa Ulaya kwenye Umoja wa Mataifa ameyasema hayo wakati wa mkutano wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Amesema mifumo imara ya kodi, sera nzuri na utawala bora ni muhimu kwa kukusanya rasilimali za ndani katika mataifa hayo yanayoendelea, kwani misaada pekee asilani haitotosheleza kushughulikia mahitaji ya nchi hizo.

(SAUTI YA THOMAS MAYR-HARTING)

Kwa mujibu wa bwana Harting wajumbe wa Muungano wa Ulaya wamechangia zaidi ya nusu ya dola bilioni 129 zilizotengwa kwa ajili ya msaada rasmi wa maendeleo ambao ni fedha zinazotolewa kwa nchi zinazoendelea na taasisi kwa ajili ya kuchagiza ukuaji wa uchumi.