Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kupungua kwa gesi chafu itokanayo na misitu muhimukwa uchumi unaojali mazingira:UNEP

Kupungua kwa gesi chafu itokanayo na misitu muhimukwa uchumi unaojali mazingira:UNEP

Nchi zinazoendelea kote duniani zinaungana na mataifa yaliyoendelea na sekta binafsi kupunguza kwa pamoja gesi inayoharibu mazingira ambayo inatokana na misitu na kuhamia haraka kwenye matumizi madogo ya gesi ya cabon na kuelekea uchumi unaojali mazingira.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira Achim Steiner faida hizi za upunguzaji wa gesi itokanayo na misitu na uharibifu wa mazingira REDD+ ndio imekuwa ajenda kubwa kwenye mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa COP 17 Alhamisi mjini Durban Afrika ya Kusini na hususani mipango ya Indonesia kutumia dola bilioni moja za ufadhili toka Norway kupunguza gesi chafu ya cabon.

Pia ameongeza kwamba ufadhili kama huo unapaswa kutumika kukuza uchumi na pia kushughulikia mahitaji  muhimu ya kuleta uwiano baina ya masuala ya ukuaji uchumi, upatikanaji ajira na usawa wa kijamii.