Msuada mpya watishia haki ya kukusanyika kwa amani Malysia

7 Disemba 2011

Kundi la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa limeonya kuwa msuada mpya kuhusu kukusanyika nchini Malaysia huenda likazuia kuwepo kwa haki ya kukusanyika kwa amani. Msuada huo unapiga marufuku maandamano kwenye mitaa na marufuku ya kuwazuia vijana walio chini ya miaka 21 kukusanyika kwa amani.

Mjumbe maalum kuhusu haki ya kukusanyika kwa amani Maina Kiai anasema kuwa sheria hizi hazikubaliki chini ya sheria ya kimataifa. Naye mjumbe kuhusu utetesi wa haki za binadamu Margaret Sekaggya anasema kuwa haki ya kukusanyika na kuandamana kwa amani inalinda haki za binadamu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud