Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya wasiwasi kwa watu wa Kordofan Kusini na Blue Nile:Amos

Hali ya wasiwasi kwa watu wa Kordofan Kusini na Blue Nile:Amos

Serikali ya Sudan imehairisha ziara ya mratibu wa masuala ya dharura wa Umoja wa Mataifa Valerie Amos ya kujadili umuhimu wa kuruhusu huduma za kibadamu kwenye maeneo yaliyoathiriwa katika majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile.

Bi Amos amesema kuwa kuendelea kuzuia huduma za kibinadamu huenda kukasababisha kuzorota kwa hali zaidi yakiwemo matatizo ya utapiamlo, ukosefu wa chakula pamoja na hatari ya kulipuka kwa mabomu ya ardhini. Bi Amos anasema kuwa kumekuwa na ripoti kuwa mashambuli ya angani siku za hivi majuzi yamehatarisha maisha ya maelfu ya watu kwenye mpaka kati ya Sudan na Sudan Kusini akiongeza kuwa kila hatua inahitaji kuchukuliwa ili kuwalinda wanaojipata kwenye mizozo.