Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu kadhaa wauawa kwenye mapigano ya kikabila Sudan Kusini

Watu kadhaa wauawa kwenye mapigano ya kikabila Sudan Kusini

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kinachunguza chanzo cha mapigano mapya ya kikabila ambayo yamesabisha vifo vya watu kadhaa na kuwalazimu wengine kukimbia makwao.

UNMISS inasema kuwa takriban watu 45 wanasemekana kuuawa na wengi kulazimika kuhama makwao kwenye jimbo la Jonglei baada ya uvamizi wa jana. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)