Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano kuhusu silaha za kibaolojia waanza mjini Geneva

Mkutano kuhusu silaha za kibaolojia waanza mjini Geneva

Mkutano wa kwanza kuhusu mkataba wa kupinga uundaji na ulimbikizaji wa zana za kibaolojia umeng’oa nanga hii leo mjini Geneva. Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton amesema kuwa Marekani inatambua hatari inayosababishwa na silaha za kibaolojia akiongeza kuwa rais wa Marekani Barack Obama amelifanya suala hilo kuwa ajenda kuu huku utawala wake ukifanya jitihada za kuzuia kusambaa kwa silaha za maamgamizi.

(SAUTI YA HILLARY CLINTON)

Vile vile mwakilishi wa Iran kwenye mkutano huo amesema kuwa Iran inapinga kuundwa kwa zana za maangamizi na kujilimbikizia silaha zikiwemo za kibalojia na kemikali.