Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanasoka mashuhuri wa Hispania aanza kampeni ya kuokoa aina ya kima walio hatarini kutoweka

Mwanasoka mashuhuri wa Hispania aanza kampeni ya kuokoa aina ya kima walio hatarini kutoweka

Mchezaji soka wa kimataifa Carles Puyol, ambaye aliiongoza timu yake ya taifa kwenye fainali zilizopita za kombe la dunia, yumo kwenye kampeni zinazoendeshwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kunusuru viumbe ambavyo vipo katika mazingira hatalishi.

Ikiwa na ujumbe maalumu usemao anza sasa kuokoa orangutans, Umoja wa Mataifa umeanzisha kampeni maalumu yenye shabaya ya kutunza kiumbe wa iana hiyo ambao anakabiliwa na changamoto ya kutoweka kwenye uso wa dunia.

Zaidi ya viumbe 66,000 wanadhania kusalia katika misitu ya Bomeo na Sumatra iliyoko nchini Indonesia, Hata hivyo idadi kubwa ya viumbe hao inasemekana tayari wamepotea.

Hivyo Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na wahisani wengine imenzisha kampeni maalumu ya kuwalinda na kuwatunza viumbe hao.