Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Migiro ataka juhudi zaidi kutokomeza ubaguzi wa rangi

Migiro ataka juhudi zaidi kutokomeza ubaguzi wa rangi

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose-Migiro amesema kuna haja kubwa kwa mataifa duniani kuongeza jitihada kukabiliana na vitendo vya ubaguzi wa rangi na unyanyasaji. Akizungumza kwenye kilele cha kuadhimisha siku ya mababu wa kiafrika, Migiro amesema kuwa mataifa ulimwenguini yanapaswa kuongeza juhudi za kukabiliana na vitendo hivyo.

Hata hivyo amepongeza hatua zilizopigwa tangu kufanyika kwa mkutano wa kimataifa miaka kumi iliyopita huko Durban ambao ulijadilia hatua za upigaji marafuku vitendo vya unyanyapaa.

Amesema wakati umefika kwa jumuiya ya kimataifa kusaka mashirikiano zaidi ili hatimaye kuondokana kabisa na mienendo inayopalilia ubaguzi wa rangi.