Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wako katika hatari kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa:UM

Wanawake wako katika hatari kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa:UM

Ripoti kutoka kwa shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNEP inaeleza kwamba wanawake hasa wanaoishi kwenye sehemu zenye milima wanakabiliwa na hatari nyingi kwa maisha yao zikiwemo za kiafya na mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na zile zinazohusiana na usafirishaji haramu wa watu.

Ripoti hiyo iliyotolewa kwenye mkutano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa mjini Durban nchini Afrika Kusini inaeleza kwamba matumizi ya teknolojia isiyochafua mazingira inaweza kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa na kuboresha maisha ya wanawake. Alice Kariuki na taarifa kamili.

(TAARIFA YA ALICE KARIUKI)