Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yataka suala la uhamiaji kuzungumziwa wazi

IOM yataka suala la uhamiaji kuzungumziwa wazi

Ripoti ya mwaka 2011 ya shirika la kimataifa la uhamiaji IOM imesema kuwa wahamiaji wanahitaji kusikizwa wakati huu ambapo kuna mjadala mkali kuhusu uhamiaji. Ripoti hiyo inaeleza kwamba hata kama umefika wakati ambapo kunashuhudiwa kuhama kwa idadi kubwa ya watu katika historia bado uhamiaji limesalia suala ambalo limeshwa kueleweka wakati huu.

Ripoti hiyo inataka kuwe na mabadiliko kuhusu jinsi suala la uhamiaji linavyochukuliwa hasa wakati ambapo misukosuko ya kiuchumi, masuala ya kisiasa na kijamii yanalizungumzia suala la uhamiaji kwa njia mbaya. Jumbe Omar Jumbe afisa wa shirika la IOM amezungumza na mkuu wa idhaa hii Flora Nducha.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)