Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Niger kupokea msaada wa $6 million kukabili tatizo la njaa

Niger kupokea msaada wa $6 million kukabili tatizo la njaa

Mfuko wa Umoja wa Mataifa uanohusika na utoaji wa misaada ya dharura umetenga kiasi cha dola za kimarekani milioni 6 kwa ajili ya kuipiga jeki Niger inayokabiliwa na tatizo la ukosefu wa chakula.

Mfuko huo wa Umoja wa Mataifa ulianzishwa rasmi mnamo mwaka 2005 kwa ajili ya kukusanya akiba ya fedha kuzisaidia nchi zinazokubwa na matatizo ya dharura. Nchi hiyo iliyoko kwenye Afrika Magharibi inakabiliwa na upungufu wa tani nusu milioni ya nafaka.

Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNICEF kwenye eneo hilo amesema kuwa vipindi virefu vya ukame pamoja na kukosekana kwa mvua za kutosha kwa baadhi ya maeneo ndiko kulikosababisha kuwepo wa mavuno hafifu.