Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ITU imetoa ripoti ya kufanya huduma ya televisheni kupatikana kwa wote

ITU imetoa ripoti ya kufanya huduma ya televisheni kupatikana kwa wote

Muungano wa kimataifa wa mawasiliano ITU umetoa ripoti mpya inayohusu upatikanaji wa huduma ya televisheni, jinsi gani ya kuifanya moja ya teknolojia maarufu duniani kuwafikia mamilioni ya watu ambao wana ulemavu unaowafanya washindwe kuona na kusikia.

Kwa mujibu wa ITU televisheni ni moja ya teknolojia inayopatikana kote duniani, huku nyumba zaidi ya bilioni 1.4 duniani zikiwa na runinga idadi ambayo ni sawa na asilimia 98 kwa nchi zilizoendelea na karibu asilimia 73 katika dunia ya tatu.

Kwa kutambua umuhimu wa runinga katika moja ya njia za mawasiliano na kufikisha taarifa kwa umma, kuelimisha na kuburudisha ITU kwa kushirikiana na mdau G3ict imetoa ripoti ya kuifanya televisheni kupatikana kwa wote, ripoti mpya ambayo imetengenezwa kwa njia ya digital ili kuwasaidia mamilioni ya watu duniani wanaoishi na ulemavu unaowafanya wasifurahie kikamilifu huduma ya televisheni majumbani kwao.