Ugiriki imevunja mkataba na Macedonia Jamhuri ya zamani ya Yugoslavia

5 Disemba 2011

Ugiriki ilivunja makubaliano yaliyokuwa yanapigiwa upatu na Umoja wa Mataifa baina ya taifa hilo na Macedonia Jamhuri ya zamani ya Yugoslavia, pale ilipozuia jaribio la jirani yake huyo la kuwa mwanachama wa NATO imesema leo mahakama ya kimataifa ya haki ICJ.

Katika uamuuzi ulioungwa mkono kwa kura 15 dhidi ya moja mahakama ya ICJ imeamua kwamba Ugiriki ilikiuka wajibu wake chini ya kifungu namba 11 cha sheria za mpito za tarehe 13 Septemba mwaka 1995 ilipopinga ugombea wa Macedonia Jamhuri ya zamani ya Yugoslavia kuingia kwenye NATO kwenye mkutano uliofanyika Bucharest mwaka 2008.

Makubaliano hayo ya mpito yaliafikiwa kama sehemu ya juhudi zilizoongozwa na Umoja wa Mataifa kutatua mvutano wa muda mrefu baina ya nchi hizo mbili dhidi ya jina muafaka la Jamhuri hiyo ya zamani ya Yugoslavia ambayo ni Macedonia.

Katika uamuzi wake ICJ pia imesema kifungu 11 kinaeleza kwamba Ugiriki imekubali kutopinga ombi lolote la kujiunga na mashirika ya kimataifa au taasisi kwa Jamhuri hiyo ya zamani ya Yugoslavia ambayo ni Macedonia labda pale tuu nchi hiyo itakapotumia jina tofauti.

Majaji wametupilia mbali madai ya Ugiriki kwamba kulikuwa na uhalali wa wao kupinga ombi hilo kwani Macedonia tayari ilishakiuka muafaka.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter