Mjumbe wa UM akaribisha hatua ya kuwepo kwa kituo cha michezo kwa vijana nchini Burundi

5 Disemba 2011
Mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa ambaye yupo ziarani barani Afrika leo ametembelea kituo cha michezo kwa vijana kilichoko nchini Burundi karibu na mpakani mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kupongeza shughuli zinazofaynika kituoni hapo.

Wilfried Lemke ambaye anazitembelea nchi za Afrika Kusini, Kenya na Burundi aliwasili kwenye kituo hicho kinachojulikana kwa jina la Gatumba na kujionea shughuli mbalimbali ikiwemo miradi inayopalilia maendeleo na amani.

Kituo hicho ambacho kinabeba matarajio ya vijana wa kiafrika ni sehemu ya mpango wa Umoja wa Mataifa kuanzisha vituo kama hivyo kwa ajili kusukuma mbele shughuli za maendeleo na amani.

Vituo vingine kama hivyo vinapatikana huko Gaza, Tajikistan na kingine nchini Ukraine kikiwa na shabaya moja ya kuwaendeleza vijana.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter