Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maonyesho ya maendeleo ya kusini-kusini yaanza Roma:FAO

Maonyesho ya maendeleo ya kusini-kusini yaanza Roma:FAO

Shirika la chakula na kilimo FAO kuanzia Jumatatu Desemba 5 ni mwenyeji wa maonyesho ya kimataifa ya maendelo ya Kusini-Kusini. Maonyesho hayo yametengwa maalumu konyesha na kushirikiana mafanikio mfano mikakati ya suluhisho la changamoto za maendeleo zinazoikabili dunia hivi sasa ambayo inaongozwa na mataifa ya Kusini.

Kwa mujibu wa FAO maonyesho ya mwaka huu ambayo huandaliwa kila mwaka na kitengo cha shirikiano wa Kusini-Kusini yanaweka bayana hali ya matatizo ya usalama wa chakula duniani ambayo inashuhudia watu zaidi ya milioni 925 wakilala njaa kila siku.

Wawakilishi kutoka nchi mbalimbali, jumuiya za kijamii, sekta binafsi na mashirika ya Umoja wa Mataifa wanahudhuria maonesho hayo yanayotarajiwa kukamilika kukamilika Desemba 9, ambayo pia yatatafuta suluhu ya muda mrefu ya matatizo ya usalama wa chakula duniani.