Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma mpya ya helikopta ina wahakikishia msaada wakimbizi wa Kisomali:WPF

Huduma mpya ya helikopta ina wahakikishia msaada wakimbizi wa Kisomali:WPF

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP limezindua huduma za helkopta ili kupeleka msaada wa chakula unaohitajika haraka kwenye makambi ya Ethiopia yanayohifadhi wakimbizi wa Kisomali.

Msaada huo wa helkopta umefanikishwa na idara ya tume ya Ulaya ya misaada ya kibinadamu ECHO, na helkopta hizo zilizoanza safari Jumatatu zitaruhusu uwezekano wa kufika katika kambi za Dolo Ado ambako ndege zingine zimeshindwa kutua kutokana na mvua kubwa. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)