FAO, IFAD na WFP wamewasaidia watu milioni 22 kwa uwekezaji wa wa kilimo wa EU

2 Disemba 2011

Katika miaka miwili tu shirika la chakula na kilimo FAO, mfuko wa maendeleo ya kilimo IFAD na shirika la mpango wa chakula duniani WFP ina watu zaidi yamesaidia watu zaidi ya milioni 22 walioathirika sana na kupanda  kwa bei ya chakula duniani.

Msaada huoni kwa hisani ya ufadhili wa kitengo cha chakula cha muungano wa Ulaya (EUFF) ambacho kimedhihirisha kwamba uwekezaji katika kilimo na lishe unaimarisha usalama wa kimataifa wa chakula yamesema mashirika hayo matatu hii leo.

Athari za gharama kubwa za chakula 2007-2008 na msukosuko wa kiuchumi na kifedha umewaingiza mamilioni katika umasikini na njaa. Hadi kufikia mwaka 2008 ambapo idadi ya watu wenye utapia mlio ilipokaribia bilioni moja muungano wa Ulaya ulizindua kitengo cha Euro bilioni moja cha chakula.

Kwa kushirikiana na jopo la Umoja wa Mataifa la kuangalia matatizo ya usalama wa chakula EUFF ilitoa Euro milioni 38 kupitia FAO, IFAD na WFP ili kuziba pengo kati ya mahitaji ya dharura na ya muda mrefu kwa kusaidia sekta ya kilimo katika uzalishaji wa kilimo kwa nchi ambazo zimeathirika sana. Kwa mujibu wa mkurugenzi wa FAO Jaques Diof kati ya mwaka 2009 na 2011 watu milioni 5 katika nchi 10 wameimarisha usalama wa chakula kwa msaada wa karibu Euro milioni 84 zilizotolewa na EUFF.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter