Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bado vitendo vya utumwa vinaendelea kwenye nchi nyingi

Bado vitendo vya utumwa vinaendelea kwenye nchi nyingi

utumwa dunianiMtaalamu huru wa masuala ya utumwa kwenye Umoja wa Mataifa Gulnara Shahidian amesema kuwa hata baada ya kuwepo jitihada za kupambana na utumwa kote duniani bado tatizo hilo limesalia kwenye nchi nyingi.

Akiongea wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupambana na utumwa anasema kuwa baadhi ya vitendo vinavyotajwa kuwa utumwa ni pamoja na ajira ya lazima, ajira ya watoto na usafirishaji haramu wa wanawake na watoto ili kufanya kazi ya malipo madogo na kudhulumiwa kingono.

Lakini pia Shahinian anasema kuwa watumwa hawajaachwa peke yao bali wanapata usaidizi kutoka Umoja wa Mataifa kupitia kwa mfuko wa UM uliobuniwa mwaka 1991. Mfuko huo unatoa usaidizi wa kibinadamu , kisheria na kifrdha ambapo pia umefadhili zaidi ya miradi 400 ya kusaidia watumwa kwenye nchi 90.