Ethiopia yafungua kambi mpya kwa wakimbizi kutoka Somalia

2 Disemba 2011

Mamia ya wakimbizi wa kisomali walio kwenye kambi ya Dollo Ado wamehamishwa kutoka kwenye kituo kilichokuwa na msongamano wa watu kwenda kwa kambi mpya ya Bur Amino. Kambi hiyo ilifunguliwa siku ya Jumatano na kuwa ya tano kwenye eneo la Dollo Ado.

Kundi la kwanza la wakimbizi 400 wamehamishiwa kambi hiyo iliyo umbali wa kilomita 26. Kwa majuma kadha sasa wasomali 7500 wamekuwa wakiishi kwenye kituo hicho kilichojengwa kuwapa hifadhi idadi ndogo ya wakimbizi na kwa siku chache. Andrej Mahecic ni msemaji wa shirika la kuhudumiia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR

CLIP

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter