Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahaka ya ICC yatoa hati ya kukamatwa kwa aliyekuwa waziri wa ulinzi wa Sudan

Mahaka ya ICC yatoa hati ya kukamatwa kwa aliyekuwa waziri wa ulinzi wa Sudan

Majaji kwenye mahakama ya kimataiafa kuhusu uhalifu wa kivita ya ICC wameomba kutangazwa kwa waranti wa kukamatwa dhidi ya waziri wa ulinzi nchini Sudan, Abdelrahim Mohamed Hussein kwa uhalifu wa kivita na uhalifu uliotendwa kwenye jimbo la Darfur tangu Agosti Machi mwaka 2003 hadi Machi 2004.

Bwana Hussein alikuwa waziri wa masuala ya ndani na mjumbe maalum wa serikali ya Sudan kwenye jimbo la Darfur wakati huo. Wanajeshi wa Sudan na washirika wao wa kundi la Janjaweed walivamia vijiji na miji magharibi mwa Darfur kwenye kampeni ya kati ya mwaka 2003 na 2004. Kiongozi wa mashataka kwenye mahakama ya ICC Luis Moreno Ocampo anasema kwa bwana Abdelrahim Mohamed alichangia pakubwa kwenye uavamizi huu.