Lazima jumuiya ya kimataifa ichukue hatua kuwalinda raia wa Syria

2 Disemba 2011

 Ripoti inayosema kuwa vikosi vya jeshi nchini Syria vimeendesha uhalifu dhidi ya ubinadamu imekuwa ikijadiliwa kwenye mkutano wa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva. Inakadariwa kuwa zaidi ya watu 4000 wakiwemo watoto 307 wameuawa nchini Syria.

Kwa upande wake mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Matiafa Navi Pillay ameitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka ili kuwalinda wananchi wa Syria.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter