Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Baraza Kuu apongeza hatua ya kutolewa ripoti juu ya uvunjifu wa haki za binadamu Bahrain

Rais wa Baraza Kuu apongeza hatua ya kutolewa ripoti juu ya uvunjifu wa haki za binadamu Bahrain

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz amepokea ripoti ya uchunguzi kuhusu madai ya kufanyika vitendo vya ukandamizwaji wa haki za binadamu huko Bahrain na akatoa mwito utekelezwaji wa mapendekezo yaliyopo kwenye ripoti hiyo

Rais huyo amepongeza uamuzi uliochukuliwa na mfalme Hamad bin Issa Al-Khalifah kuunda kamishna huru ambayo itawajibika na utekelezwaji wa mapendekezo yaliyotolewa na ripoti hiyo.

Timu hiyo ya uchunguzi iliongozwa na Professor Cherif Bassiouni,imebaini kuwepo kwa uvunjifu wa haki za binadamu wakati vikosi vya serikali vilipoendesha operesheni ya kuyasambaratisha maandamano ya amani.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekaribisha ripoti hiyo na ameitolea wito serikali ya Bahrain kutilia maanani yale yaliyopo kwenye ripoti hiyo.